Msajili wa vyama Jaji Francis Mutungi. Nimefanya naye kazi kwa karibu tangu tunaandikisha chama mpaka tunapata usajili wa kudumu na kuendelea nikiwa Katibu Mkuu wa chama hicho kipya. Jaji Mutungi ni mtu mcheshi sana. Mkikutana mahali ambapo si ofisini halafu mtu akaja hapo na kuwakuta mnapiga stori na Mutungi, anaweza asijue bosi ni yupi. Ni mpole, rafiki wa watu, mvumilivu sana, mtu chanya (hafikirii mabaya wakati wote anatumaini mambo yatakuwa mazuri), mpatanishi, mwenye malengo makubwa, nk. Kwenye mgogoro wa uongozi kwenye chama nilichokuwa nakiongoza, nilimfahamu kwa ndani Mutungi. Amekuwa rafiki yangu mpaka leo. Kwa jinsi alivyo ‘social’ mpaka leo nimeacha uongozi lakini wakati wowote nampigia simu Mutungi kama ana nafasi tunaongea, tunabadilishana mawazo. Ukimwambia Mutungi jambo ambalo unaona ni gumu na kwamba watu wanamshambulia sana, atakuambia, "Hawajaelewa tu Mwigamba, na kazi yetu sisi ni kuwaelimisha watafika mahali wataelewa na kila kitu kitakuwa sawa".
Ni sifa hizi ndizo zimemfanya awe Kikwete wa pili wa CHADEMA. Wanamchezea wanavyotaka na hata kumdhihaki, kumchafua na kumdhalilisha. Nilicheka sana niliposoma majibu ya Mnyika kwa Msajili wa vyama. Utadhani hana wanasheria wa kumshauri kumbe wanapotosha ukweli kwa makusudi. Msajili anawapa vifungu vya sheria ya vyama inayohusu mambo ambayo chama kikiwa kinayafanya hakiwezi kupata usajili. Wao wanamwambia kwani sisi tunataka usajili ? Wanasahau kwamba kisheria chama kikifanya jambo ambalo kingefanya kabla hakijasajiliwa kingekosa sifa za kusajiliwa, basi huwa kinafutwa. Kama vile tu ambavyo kuna sifa za mtu kuwa mbunge kama Mnyika na sifa hizo ukizikosa ukiwa mbunge unapoteza ubunge. Yaani kama ulichaguliwa kuwa mbunge wa Kibamba ukiwa na akili timamu kama sifa mojawapo, leo ukiwa mbunge ukakosa akili timamu ukawa kichaa, unapoteza huo ubunge.
CHADEMA kwa sasa ina mambo mengi sana ambayo kama ingekuwa nayo kabla ya usajli isingesajiliwa. Mambo hayo ni pamoja na kumilki jeshi lake linaloitwa Red Brigade ambalo linafanya kazi za ulinzi na kushambulia na mifano ipo kuanzia Igunga mpaka Kinondoni, CHADEMA inahamasisha vurugu na kutamka waziwazi kuwa tayari kupoteza maisha ya watu 100 hadi 200, inahamasisha uasi wa sheria hadi kutaka kuiangusha serikali iliyoko madarakani bila kutumia sanduku la kura, inafanya siasa za fujo na vurugu ikiamini ndizo zitakazoifikisha madarakani, imewahi kuchochea kuvunja muungano kupitia kwa kiongozi wake mmoja Tundu Lissu, na nyingine nyingi zinazomtaka kwa kweli msajili wa vyama akifutie usajili chama hicho. Lakini kwa upole wake, kwa wema wake, kwa matumaini yake anaendelea kuamini itafika siku watajirekebisha na wao ndio wanazidi kumchafua.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)