Bendera ya Tanzania yazua Utata

Maafisa wa Ugiriki wanaofanya doria baharini wamesema wanaishikilia meli iliyokuwa inapeperusha bendera ya Tanzania inayodaiwa kubeba zana za milipuko.
Meli hiyo inadaiwa kusafirisha milipuko hiyo kutoka Uturuki kwenda Libya, kinyume na sheria iliyopiga marufuku ya kusafirisha silaha kwenda nchini Libya.
Maafisa wanasema meli hiyo ilikuwa imebeba kreti 29 zilizojaa zana hizo pamoja na kemikali.

Related image