UTEUZI: Rais Magufuli afanya Uteuzi wa mabalozi wawili

Rais Magufuli amemteua Alphayo Kidata (Pichani) kuwa Balozi.
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Alphayo Kidata umeanza tarehe 10 Januari, 2018.

Kabla ya uteuzi huo, Alphayo Kidata alikuwa Katibu Mkuu, Ikulu.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Meja Jenerali Mstaafu Simon Mumwi kuwa Balozi.
Mabalozi hawa wateule watapangiwa vituo vya kazi na kuapishwa baada ya taratibu kukamilika.

Image may contain: 1 person, suit
Alphayo Kidata