Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla awasili Mkoani Morogoro kwa ziara Maalum ya siku mbili kwenye bonde la Kilombero ambalo ni chanzo kikubwa cha maji yanayotengeneza Stiegler’s Gorge ambako Serikali ya Rais Dkt. John Magufuli inatekeleza mradi wa kihistoria wa kuzalisha umeme wa megawatts 2100.
Uhai wa bonde hili si tu ni mafanikio ya mradi huu bali pia ni uhai wa hifadhi kubwa ya wanyama aina ya sheshe na ndege zaidi ya aina 400, pia mazalia ya samaki wa bahari ya hindi wanaozalia maji baridi kwenye mto Rufiji. Bonde hili lilitelekezwa siku nyingi na hivyo kuvamiwa kwa kishindo kikubwa na wakulima na wafugaji.