JAFFO AONYA MATUMIZI YA WHATSAPP KWA WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jaffo leo ameawataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuwa makini na siri za Serikali, husasan dhidi ya kuvujisha katika mitandao ya kijamii.
Akifungua mafunzo ya maadili kwa viongozi wa umma mjini Dodoma leo Januari 29,2018 Jaffo amewaambia viongozi hao kuwa utendaji wa serikali utaimarika zaidi iwapo watakuwa makini na kutunza siri.
“inastaajabisha kwa kweli, unakuwaje wewe mkurugenzi au mkuu wa wilaya halafu unapeleka siri za Serikali kwenye mitandao ya kijamii? Na nyingi utaziona kwenye WhatsApp, inatia aibu sana."
Image may contain: 1 person, smiling, standing and suit