Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Majaliwa Kassim Majaliwa, amesema Serikali imeamua ujenzi wa viwanja vyote vya ndege vinavyojengwa hivi sasa vitasimamiwa na wakala wa barabara nchini Tanroads baada ya kuridhisha kuwa wakala huyo kuwa na uwezo mkubwa wa kusimamia kazi hiyo na hivyo kuipunguzia serikali gharama.
Waziri mkuu ametoa kauli hiyo mjini Musoma Mkoani Mara,baada ya kupokea taarifa za upanuzi wa ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Musoma,kikiwa ni miongoni mwa viwanja kumi na moja vya ndege ambavyo vipo katika mchakato wa ujenzi wake.
Amesema ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Musoma kwa kiwango cha lami ni sehemu ya mkakakati wa serikali wa kuimairisha usafari wa anga hasa wakati huo wa ujenzi wa Tanzania ya viwanda lakini pia ni sehemu ya kukuza sekta ya utali nchini.
Kwa sababu hiyo Mh Majaliwa,amesema tayari wizara ya maliasili na utali imeagizwa kuanzisha mamlaka ya kuesimamia Fukwe za Bahari,Maziwa na Mito ili fukwe hizo zitumike katika kukuza sekta ya utalii nchini.
Awali meneja wa Tanroads mkoa wa Mara Mhandisi Ngaile Felix Mlima,akitoa taarifa za ujenzi wa uwanja huo kwa Waziri mkuu,amesema taratibu za kumpata mkandarasi bado zinaendelea na kwamba uwanja huo utajengwa kwa awamu ya tatu kwa kuhusisha njia ya kurukia ndege,ujenzi wa jengo kubwa la abiria na uwekaji wa taa.