Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma, anazidi kukabiliwa na shinikizo la kumtaka kujiuzulu kufuatia mazungumzo na maafisa wa ngazi ya juu katika chama chake cha ANC yaliyofanyika jana Jumapili.
Hata hivyo taarifa zaidi kuhusu mazungumzo hayo hazijawekwa wazi, lakini viongozi wa chama hicho wameitisha mkutano wa dharura unaotarajiwa kufanyika leo, Jumatatu.
Zuma ambaye amerithiwa nafasi yake ndani ya chama cha ANC na, Cyril Ramaphosa anayekabiliwa na tuhuma za rushwa.
Wachambuzi wanasema wakuu wa chama hicho wanajaribu kuepuka mgawanyiko ndani ya ANC kabla ya uchaguzi mkuu mwakani.
Wanatarajiwa kuanza mchakato wa kumuondoa rais Zuma Kwa kufuata mfumo rasmi au kwa kuwasilisha hoja bungeni.