TUME YAMJIBU MWENYEKITI CHADEMA

TUME YAMJIBU MWENYEKITI CHADEMA: “Malalamiko yaliyotolewa na Freeman Mbowe yametusikitisha kwa sababu mbali na kumjibu kwa barua, Mkurugenzi wa Uchaguzi aliongea na Mbowe kwa njia ya simu.
"Madai kwamba tume haikuwajibu malalamiko yao siyo ya kweli, na ni upotoshaji wa hali ya juu." Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, Tume imesema kama majibu ya tume hayakuwafurahisha, CHADEMA watambue kuwa Tume iliwajibu kwa matakwa ya sheria na katiba na siyo matakwa ya mkurugenzi wa uchaguzi, Tume, Chadema au chama chochote cha siasa.
Image may contain: 1 personImage may contain: 1 person