Dkt. Azaveri Lwaitama: Kuna kikundi cha watu kinaendesha Serikali. Rais adhibitiwe!

Anasema ukiwa na mtu ambaye sio kiburi, sio mbabe sawa kama Nyerere sawa .

Rais kuteuwa wakurugenzi inakuwa sio uchaguzi ni uchafuzi.

Wananchi wanahitaji maendeleo ndani ya uhuru sio maendeleo bila uhuru yaani wawe kama wanaswagwa vile.

Chama ni chombo cha kushawishi sio kutisha watu, sijui usipo chagua chama hiki hutopata maendeleo..kifupi mzee wa frustration hatoipenda hii.


Inabidi tutofautishe kati ya dhana tatu;

i) Dhana ya Maendeleo: Wananchi wanahitaji maendeleo, lakini maendeleo ni maendeleo ndani ya Uhuru. Sio Maendeleo wakiwa wanaswagwa kama mateka, vingnenvyo wangewatafuta Wajapani Wajerumani waje hapa wawapige bakora ili wawe na majengo. Wananchi wanataka maendeleo ya watu, maendeleo ya kupata uhuru zaidi.

ii) Dhana Dola: Je ni dola ya kuchukulia watu mateka au ni dola la wachi huru amabo wamelidhia mamlaka fulani kwa watu ambao wanafanya kwa niaba yao?.

iii) Dhana ya Chama: Chama ni kitu kinachoshawishi, ni chombo cha kushawishi watu sio cha kuwatisha. Sio chama kinachosema usipochagua huyu maendeleo hayatakuja kwako, usipochagua huyu utashughulikiwa. Kikifanya hivyo sio chama tena bali chama dora. Ni kikundi cha watu kimekamata dola halafu kinatumia chama. Sio chama kuwashawishi watu bali kuwatisha kwa sababu watu wanataka kubaki hapo hapo walipo.

Hoja hapa ni kwamba ukishafika mahali ambapo chama kilichokuwa cha ukombozi, kimejigeuza kikawa chama Tawala "Sio mimi nasema ni wao wenyewe wanasema chama Tawala". Mimi nashangaa, baada ya kupata uhuru hakuna anayetakiwa kutawaliwa, aanatakiwa kuongozwa tu. Na kiongozi hawezi kutawala watu, anawaongoza tu kwa ridhaa yao.

Mkwaruzano hapa ni kupata katiba mpya ni katiba mpya inayopunguza mamlaka ya rais. INayoongeza nafasi ya wananchi wenyewe kusimamia mambo yao bila kutegemea mtu mmoja. Ni katiba ambayo yenye maudhui ambayo teuzi za rais lazima zipitishwe bungeni ziidhinishwe na watu wanaotokana na walichaguliwa. Iwe katiba ambayo mamlaka ya rais yanaweza yakahojiwa kutakapokuwa kumetokea uchaguzi. Mambo yote hayo ndiyo yanaitwa katiba mpya. Madai ya katiba mpya sio tu itangazwe kesho kwamba hii ni katiba mpya hapana, tunauliza ni maudhui gani? Je rais teuzi zake zimepunguzwa? Je Mihimili mingine uteuzi wake hauhusiani kabisa ba rais? Je Mamlaka imegatuliwa na Wilaya inaongozwa na watu waliochaguliwa?

Kenya inafanya hivyo, Mtu anayesima na kusema Wilaya fulani inahitaji kitu fukani ni mtu aliyechaguliwa na watu wa sehemu husika. Inayezungumza Wilaya ya Ireje inataka nini, awe ni mtu aliyechaguliwa na watu wa Ireje. Sio mtu aliyeteuliwa. Mtu aliyeteuliwa ni mratibu tu. Hiyo ndio maana ya katiba mpya. Katiba mpya sio neno. Watu wanadai.


Dhana ya maendeleo.

Kama watu wanataka kujiletea maendeleo sio kuletewa maendeleo na mtu. Wanataka nafasi ya wao kuamua leo tutachangishana hivi, kesho tutachangishana hivi, hela yetu ikichangishwa hivi itatumika kwenye hiki, hiki kitangoja kesho hiki kitangoja keshokutwa. Tunataka Katiba yenye maudhui hayo.

Tunataka katiba ambayo itapunguza uwezekano wa mtu mmoja au kikundi cha watu mahali kuwafanya wananchi ni mateka, watu ambao wanatafuta hisani. Yaani maendeleo ni hisani ambayo inatolewa na mtu akipenda. Yaani maendeo yanatolewa kama mtu amefurahi. Kutoka ngazi za juu mpaka ngazi za chini. Yaani na mkuu wa Wilaya na yeye anaweza akaamua.

Wananchi wananaandamana mbele ya Waziri mkuu wanasema ondoka na huyu mkuu wa Wilaya. Manake wamefika mahali huyu mkuu wa Wilaya ndie anawaamulia wanataka nini. Sasa wao wamepata uhuru miaka zaidi ya 50, walitegemea Mkuu wa Wilaya ni mtu ambaye ni Mratibu wa shughuli za Serikali. Ni mtu ambaye anawasikiliza wao.