Kilimo cha Mananasi na masoko yake Tanzania - USHAURI

Jana niliwasilisha mkusanyiko wa mada zinazohusu ufugaji wa kuku..

Leo naomba niweke mkusanyiko wa mada za kilimo.. nimeamua kufanya hivi ili kusaidia wale ambao ni wanachama wapya na wanachama wengine ambao wanataka kujikumbusha mada hizo na kuchukua hatua:

ARDHI
Ardhi ya kilimo: Ardhi ya kilimo
Ardhi ya kilimo!!! Natafuta ardhi ya kilimo ya bei nafuu
Shamba kwa ajili ya kilimo Shamba kwa ajili ya kilimo
Ardhi ya kilimo Tsh 5000 kila Ekari ya mbuga Ardhi ya kilimo Tsh 5000 kila Ekari ya mbuga
Ardhi kwa Kilimo cha Kitunguu Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na masoko
MAZAO
Mazao gani yanafaa kwa kilimo chalinze? Part 1 Mazao gani yanafaa kwa kilimo chalinze?
Mazao gani ya kilimo yanastawi maeneo ya chalinze? Part 2 Mazao gani ya kilimo yanastawi maeneo ya chalinze?
Kilimo cha Mitiki: Utaalamu Kilimo cha Mitiki: Utaalamu na biashara yenyewe
MIKAKATI KATIKA KILIMO
kilimo-wakulima wa jf getting together Wakulima wa JF getting-together
Kilimo kwanza initiative: Nasaidiwaje na serikali/taasisi za serikali? Kilimo kwanza initiative: Nasaidiwaje na serikali/taasisi za serikali?
Power tiller na dhana ya kilimo kwanza Power tiller na dhana ya kilimo kwanza
Kwanza Kilimo? https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/31557-kwanza-kilimo.html
Kwa Wajasiriamali hasa wa sekta ya Kilimo... Kwa Wajasiriamali hasa wa sekta ya Kilimo...
haya ndo nimeweza kukusanya kwa leo.. hopefully hii itasaidia kutoa mwanga kwa wale wanaotaka kuperuzi posts mbalimbali..


tukumbuke!! TUKIWEKA JITIHADA.. KILIMO KINALIPA!!.nawapeni mfano: unaenda Kiwangwa bagamoyo unanunua ekari moja ya ardhi kwa ajili ya kilimo cha nanasi.



Gharama zitakuwa hivi:
ununuzi wa ardhi kwa Tsh. 300,000-- (ekari ni hatua 70x70)
utayarishaji wa shamba Tsh 150,000/=
gharama ya miche na upandaji miche 15,000 kwa ekari Tsh 750,000 (i.e.50 x 15,000 ikijumuisha ununuzi wa mbegu na upandaji),
Mbolea 100,000.
matumizi mengine 200,000 (ikiwa ni pamoja ni vibarua, na kuleta mzigo sokoni).
jumla 1,500,000/-
Mapato
nanasi unavuna baada ya miezi 18. kwa hesabu za chini kabisa unauza nanasi moja kwa Tsh 500 na assume unapata nanasi 12,000 utapata Tsh 6,000,000/=. (assumption ni kuwa si rahisi kupata mavuno 100%- bali inaweza kuwa 80%)

Faida :
ukiondoa matumizi (Tsh 1,500,000) unapata faida 4,500,000 ukiwa na ekari tano bila shaka utapata zaidi ya milioni 20 (na hapo hujaweka economy of scale). --though unaweza kupunguza au kuongeza asilimia fulani kutegemeana na risks zilizopo na uzoefu wako katika kusimamia na kutafuta masoko..

soko likoje
Kuna atakayeuliza je soko lipo-- mimi nasema soko lipo huko huko shamba au unaleta kwa BAKHRESA anayenunua matunda kwa ajili ya kutengeneza natural juice i.e. azam box juice). nasikia kuna kiwanda kingine kinaanzishwa bagamoyo (siyo bakhresa). ila tukumbuke kwa sasa ambapo nanasi ni chache ukienda sokoni huwezi pata nanasi chini ya 1,500/-

Mfano hai
Kamuulize ndugu Eric Shigongo mambo anayofanya Kiwangwa na anapata nini?-

Mwenye taarifa zaidi au anayetaka kukosoa ni vema amwage hapa..