Mafanikio ya Biashara si kitu Cha kitoto hata kidogo na some time huchukua hata miaka 20 ila kikubwa ni kutokata tamaa kamwe.
Vile vile Mafanikio yanahitaji Vitu Vingi sana, Kama Vile:
1. PESA
2. RASILIMALI WATU
3. SAPOTI YA NDANI NA NJE
Mimi nitajikita kwenye Sapoti ya Mwenza wako katika Kufanikisha Safari, Partner wako ana mchango mkubwa sana wa hadi 40% katika kufanikisha safari yako, mchango wake sio tu wa kukusaidia kazi no bali hata kukutia moyo mara kwa mara na kuwa sehemu ya mafanikio yako na kuchukulia matatizo yako kama yake.
Mara Nyingi sana tumekuwa tunaingia kwenye Ujasirimali ambapo utakuta Mzee yuko Bize na Kilimo, Ila mama ishu za kilimo yeye kwake hazipandi kabisa, mama yuko bize na Ufugaji lakini mzee yeye maswala ya kufuga kwa kweli sio.
Unaanzisha Biashara ya Hoteli, Ila mama yeye yuko bize na kazi na ishu za hotelini hazijui au vise verse. Kwa kweli kwa staili hii ni Vigumu sana kuja kufanikiwa take it from me.
Unapokuwa wewe unapenda Kilimo lakini ndani ya nyumba mwenzako yeye anapenda biashara ya saloon au anapenda duka sijui la Nguo, inakuwa ni ishu sana nani atamtia moyo mwenzake?
Mara nyingi sana nimekuwa nikienda Kenya kwe kweli moja ya mambo niliyoyaona ni hili la wote wawili kuwa bega kwa bega katika kitu kimoja, Jamaa ukikuta mi Ufugaji basi mama anajua A-to Z na yeye ndo Meneja masoko au ndo sales meneja kama ni kilimo utakuta ni bega kwa bega, wote wanalima na wote wanajua kilimo kilivyo, kiasi kwamba mmoja akiugua hata mwezi mzima kazi zinaenda kama kawaida.
Ukikuta wewe mfano Unafuga Kuku alafu Mke/mme anachukulia ule ufugaji kama kinyaa na hawezi hata kuingia bandani kwa kuogopa kinyesi cha kuku basi tambua kwamba kuja kufanikiwa ni vigumu sana tena mno.
Ukikuta wewe unapenda kilimo na una mashamba makubwa lakini mwenzako hajui hata jembe linashikwa vipi au hajui hata watu wanaoteshaje mazao basi tambua kuja kufanikiwa ni vigumu sana.
Partner wako ana mchango mkubwa sana katika kufanikiwa kwako, pale atakapokuwa sehemu ya project yako, pale atakapo jua A to Z za project yako.
Mkisha kuwa ndani ya Nyumba mna-intrest tofauti inakuwa ni kazi sana kuja kufanikiwa, mmoja anapenda kilimo, mwingine hapendi, na time ikitokea ukaugua au ukasafiri au ukapata ishu kubwa au hata kufungwa ndo pale unakuta kila kitu kimerudi kama mwanzo, kwa sababu wewe ulikuwa na project ya shamba lakini mwenzako yeye anaogopa sana kukanyaga tope au kuchafuka au hata kwenda tu shamba so ukiugua ndo basi.
Hivyo Pale mnapokuwa wote mna-interest Moja inakuwa ni vizuri sana na mafanikio huonekana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)