Rais Yoweri Museveni Jumapili aliwafuta kazi mkuu wa polisi Jenerali Kale Kayihura pamoja na Waziri wa Usalama wa Nchi Jenerali Henry Tumukunde.
Katika taarifa kwa njia ya Twitter Rais alisema anamteua Elly Tumwine kuwa Waziri wa Usalama na Okoth Ochola kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP).
“Kwa mamlaka niliyopewa na Katiba, nimemteua Jenerali Elly Tumwine kuwa Waziri wa Usalama. Nimemteua Okoth Ochola kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi na atasaidiwa na Brigedia Sabiiti Muzeei,” ilisema taarifa ya Rais.
Jenerali Kayihura, kuna wakati alifikiriwa kuwa ofisa wa jeshi mwenye nguvu zaidi nchini lakini hivi karibuni alipishana na Museveni ambaye ametawala Uganda tangu alipotwaa madaraka ya nchi akitokea msituni mwaka 1986.
Kayihura aliteuliwa kuwa IGP mwaka 2005, mwaka ambao kura ya maoni ilipitishwa kwa mafanikio kurejesha mfumo wa demokrasia ya vyama vingi baada ya kupigwa marufuku kwa miaka 20.
Utawala wake ulionekana ukitumia zaidi mbinu za vitengo vya kijeshi na vilevile ilienea dhana kwamba siasa iliingia katika jeshi hilo la polisi.
Tangu Machi 2017 yalipofanyika mauaji ya Felix Kaweesi, polisi mwandamizi ambaye alikuwa anatazamwa kama mrithi wake mwenye uwezo, Kayihura amekuwa akikabiliwa na presha kubwa kwa kushindwa kwake kuzuia ongezeko la ukosefu wa usalama.
Wanawake wapatao 23 wameuawa katika mauaji ambayo ufumbuzi wake haujapatikana na yasiyojitenga karibu na mji mkuu, kumekuwa na jeraha la vifo vya wananchi wa kigeni na juma jana mwanamke kutoka familia yenye ushawishi aliuawa baada ya kufungwa kwa wiki tatu kwa watoa nyara wanadai fidia kubwa.
Rais, ambaye mara kwa mara amekuwa akisisitiza kuwekwa kamera za CCTV katika maeneo ya mijini kama njia ya kupambana na uhalifu, hivi karibuni aliongeza kuwa ni wakati wa kutumia utambulisho wa viganja na vipimo vya DNA ili kusaidia kupambana na uhalifu.
Chanzo: Mwananchi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)