Shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto, UNICEF limesema kuwa kuna mafanikio makubwa ya kupungua kwa ndoa za utotoni duniani.
Shirika hilo la Unicef limekadiria kuwa ndoa za utotoni zipatazo milioni 25 zimeweza kuzuiliwa katika muongo iliyopita.
Kwa sasa ni msichana mmoja kati ya watano anaoewa chini ya miaka 18 tofauti na miongo iliyopita ambapo ilikuwa msichana mmoja anaolewa kati ya wanne.
Shirika hilo la watoto limesema Kusini mwa nchi za bara la Asia wamejitahidi zaidi katika kupunguza ndoa za utotoni.
Anju Malhotra, mshauri wa masuala ya jinsia kutoka Unicef anasema haya ni mabadiliko mazuri katika maisha ya wasichana wote duniani hivyo upunguaji wa vitendo hivyo hata kwa kiwango kidogo ni habari njema ingawa bado kuna safari ndefu ya kutokomeza ndoa hizo za utotoni.
Ripoti hiyo imeeleza kuwa nguvu kubwa ya kutokomeza tatizo hili la ndoa za utotoni ilihamia Afrika,ambapo jitihada zaidi zilihitajika ili kupunguza tatizo hilo.
Kwa sasa ripoti inaelezwa kuwa ndoa moja ya utotoni inafungwa kati ya ndoa tatu katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara wakati miongo iliyopita ilikuwa ndoa utotoni moja kati ya ndoa tano za utotoni.
Hata hivyo jitihada za matokeo ya mabadiliko haya ni kutokana na kampeni nyingi zilizofanywa duniani ingawa bado changamoto zipo katika kufikia lengo hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)