Jacqueline Wolper matatani tena mchumba aliyemtambulisha kwa jina la Leonard

Msanii mwenye mikasa mingi, Jacqueline Wolper ainadaiwa kuwa amepatwa na taharuki baada ya Jana tarehe 14 kugundua kuwa mchumba aliyemtambulisha kwa jina la Leonard kuwa alishaoa miezi mitatu (3) iliyopita.
Mcheza Filamu huyo ambaye alishajiaminisha kufunga ndoa na mwanaume huyo, amepatwa na mshtuko huo huku wakiwa tayari wameshajipanga mwezi ujao, kwenda kukamilisha taratibu za kujitambulisha kwa wazazi wa Wolper.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Wolper amesema, alidhani amempata mwanaume sahihi kumbe siyo na kwamba, anasikitika kwa kitendo hicho cha kudanganywa.
Image may contain: 1 person, close-up
"Ninasikitika kwani nilichanga pesa zangu kwaajili ya kumuongezea jamaa kununua taxi ili kufanya biashara kama wanandoa watarajiwa kumbe mwenzio kashaoa bila kuniambia."
Wolper amewaalaani wote waliofahamu hilo na kukaa kimya pamoja na mwanamke wa jamaa na huyo aliyemuoa kwa kusema muda aliopoteza na machozi yake hayataenda bure.