Polisi nchini Guinea wanamshikilia mwanamama anayedaiwa kuwa ni mponyaji kwa makosa ya kuwadanganya mamia ya wanawake kuamini kuwa wanapata mimba kimiujiza.
N'na Fanta Camara amekuwa akiwapa wanawake ambao hawajaweza kubeba mimba majani mchanganyika ambayo husababisha matumbo yao kujaa na kuonekana kama mimba.
Ili kupata huduma yake, mgonjwa anatakiwa kulipa Dola za Kimarekani 33, katika nchi ambayo mshahara wa kawaida kwa mwezi ni dola 48.
Polisi wanaamini kuwa Camara amekuwa akijitengenezea maelfu ya dola katika mwezi licha ya mwenyewe kusema kuwa alichokuwa akifanya ni kuwasaidia wanawake hao.
Jumanne , wanawake zaidi ya 200 waliandamana na kukusanyika nje ya kituo cha Polisi katika mji mkuu wa nchi hiyo Conakry ambapo mwanamama huyo anashikiliwa.
Zaidi ya wanawake 700 wenye umri kati ya miaka 17 hadi 45 wanaaminika kuathiriwa na ‘matibabu’ ya mimba ya Camara