Watu wasiojulikana wamechoma nyumba ya Katibu wa Umoja wa Vijana CCM

Watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo, wamechoma nyumba ya Katibu wa Umoja wa Vijana CCM wa Mkoa wa Iringa, Alphonce Muyinga iliyopo maeneo ya Kihesa njiapanda ya Kwabeda.
Mbali na uhalifu huo, naye aliyekuwa diwani wa CHADEMA, Anjelus Mbogo, ambaye hivi karibuni alitangaza kujiuzulu, nafasi hiyo amekutana na tafrani ya kubomolewa nyuma yake iliyokuwa katika hatua ya ujenzi iliyopo Igumbilo na watu wasiojulikana.