Magufuli apiga Marufuku Michango Mashuleni

Rais Dkt Magufuli akutana na mawaziri wa Elimu na Tamisemi, apiga marufuku michango Mashuleni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekutana na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani S. Jafo na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce L. Ndalichako Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 17, 2018. Mhe. Rais amepiga marufuku aina yoyote ya michango katika shule za serikali za msingi na sekondari na amewaagiza mawaziri hao kusimamia hilo.