Kamanda Mambosasa asema waliopata msamaha wa Rais waache kufukua silaha

Kamanda wa Polisi, Lazaro Mambosasa asema kuwa walitoka jela kwa msamaha wa rais wabadili tabia na fikra. Awaonya kuwa wasirudi kufukua silaha na kurudi kwenye uhalifu, Jeshi la Polisi haitawaacha salama

Wapo Watu walioko jela wanawatuma watu waende wakafukue Silaha ili zitumike katika matukio ya uhalifu. Watu hao wanadai wapelekewe posho zilizotokana na matumizi ya silaha hizo

Asema kuwa watuhumiwa waliokamatwa na silaha wamedanganya kuwa wameziokota kwenye vyuma chakavu

KAMANDA Mambosasa pia amesema kuwa Jeshi la Polisi limemkamata Mwanaume aliyeuwa Familia yake kwa kutumia Jembe. Mwanaume huyo alimuuwa Mke wake, Mtoto wa miezi minne na Shemeji yake.

Mwanaume huyo amekamatiwa Mkoani Iringa na sasa anasubiri uchunguzi ukamilike ndipo afikishwe mbele ya vyombo vya sheria