Mahakamani kwa tuhuma za kumbaka Mbuzi

Mtu mmoja nchini Kenya mwenye umri wa miaka 35 amefikishwa mahakamani akituhumiwa kubaka mbuzi wawili wa jirani yake na kisha kuwaua. Tukio hilo limetokea Januari 13 mwaka huu, baada ya watu kumuona akiwaburuza mbuzi hao kutoka porini ambako anahisiwa kufanya tukio hilo.

Waendesha mashtaka wametaka mbuzi hao wapelekwe kufanyiwa vipimo ili kubaini kama kweli wamefanyiwa kitendo hicho, na kutaka mshtakiwa kupatiwa matibabu baada ya kulalamika alipigwa vibaya na polisi walipoenda kumkamata.

Sheria za Kenya zinamtaka mtu atakayekutwa na hatia ya kufanya ukatili kama huo kwa wanyama kwenda jela kwa miaka 14.

Image may contain: outdoor and nature