Nifungua Jeneza na Kisha nikajiona Mwenyewe...


Kijana mmoja aliota kwamba nyumbani kwao watu wana fanya maandalizi ya mazishi.

Lakini katika kuota kwakwe akawa hajui nani aliye kufa. Ikabidi aende jirani na mzee mmoja wa makamo na kumuuliza "samahani mzee hapa ni kwetu lakini naona watu wanalia na wengine wanafanya maandalizi ya kwenda kuzika. Kwani alie kufa ni nani?

Mzee akajibu nenda kwenye jeneza kaangalie mwenyewe. Kijana kuangalia kajikuta yeye ndo yuko kwenye jeneza na ndo alie kufa.

Akapiga kelele kubwa na kuwaambia waombolezaji Jamani msilie wala msiende kunizika Mimi niko hai. Lakini wakamjibu umesha chelewa lazima uzikwe. Mara akazinduka usingizini akiwa na hofu kubwa huku akitetetemeka kwa hofu.

Akajipa moyo na kupiga magoti na kumuomba Mungu hivi.

Baba, kama Kuna mtu anatafuta kuniua basi shughulika nae. Anarudi kitandani akalala. Asubuhi anapokea simu kuwa mama yake mdogo amefariki dunia. Kumbe alitakiwa kutolewa msukule kijana yule.

Sasa nakwambia wewe unaye soma simulizi yangu hii, mwaka huu 2018, Mchawi yeyote atakaye nyoosha mkono wake juu yako kwa ubaya Mungu atashughulika nae haraka.