Nikivaa viatu nahisi kupoteza ‘network’ - Mrisho Mpoto

Mrisho Mpoto : Nikivaa viatu nahisi kupoteza ‘network’
Picha ya msanii wa nyimbo za asili, Mrisho Mpoto ilimwonyesha amevaa viatu imezua gumzo kwa mashabiki huku wengine wakisema kuwa msanii huyo amechoka kutembea peku peku.
Mrisho Mpoto ametoboa siri kuwa ameshindwa kuvaa viatu baada ya kujaribu mara kwa mara na kwamba picha hiyo ni ya zamani na ina miaka zaidi ya miaka 17 iliyopita.
Amesema kuwa alijaribu kuvaa viatu baada ya maneno ya watu kuzidi na kusema kuwa aliambiwa na mganga wake asivae viatu lakini alishindwa kwani akivaa anaona kama anapoteza network ila akikanyaga chini anajiona kama binadamu tofauti na akivaa viatu.
Image may contain: 1 person, standing and indoor