Tani 95 za Samaki waliokamatwa kupigwa Mnada


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ameagiza kupigwa mnada kwa zaidi ya tani sitini na tano za samaki waliokaushwa aina ya Sangara ambao walikamatwa hivi karibuni katika kisiwa cha Rubili wilayani Muleba Mkoani Kagera.

Samaki hao wakamatwa wakiwa wamehifadhiwa katika magunia tayari kusafirishwa, kinyume na sheria ya uvuvi namba ishirini na mbili ya mwaka 2003,huku mmiliki wake akitokomea kusikojulikana.