KIGWANGALLA AITEMBELEA FAMILIA YA AKWILINA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla mapema jana alitembelea nyumbani kwa familia ya Akwilina na kutoa pole kwa wafiwa.

“Nimefika hapa kama raia mwema tu ambaye nimeguswa na msiba huu na nimetafakari kwani na mimi kipindi fulani nilipitia chuo hasa kutoka familia zetu hizi masikini kwa hiyo inapotokea tukio kama ili unaona ni pigo kwa familia, pigo kwa jamii, pigo kwa wanafunzi wenzake na pigo kwa taifa kwa ujumla wake" alieleza Dkt. Kigwangalla wakati akizungumza na vyombo vya Habari msibani hapo.Image may contain: 4 people, people sitting and wedding

Dkt. Kigwanalla ambaye alifika msibani hapo majira ya saa saba mchana, aliweza kuungana pamoja na ndugu na jamaa wa wafiwa ambapo pia alipata chakula cha mchana pamoja na waombolezaji wengine sambamba na kutoa ubani wake kama mwananchi mwingine.Image may contain: 1 person, selfie and close-up