Rais Dkt. John Magufuli amewajulia hali Maria na Consolata Mwakikuti.

Rais Dkt. John Magufuli amewajulia hali baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam wakiwemo Mzee Kingunge Ngombale Mwiru na Mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti.

Maria na Consolata wamemshukuru Rais Magufuli kwa kwenda kuwaona na kuwapa pole na pia wameongoza sala ya kumuombea Rais Magufuli na nchi kwa jumla.

Image may contain: 1 person, indoor