Stoke City imemfuta kazi aliyekuwa kocha wake Mark Hughes

Baada ya kipigo kutoka timu ya daraja la pili ya Coventry City kwenye mchezo wa kombe la FA, timu ya Stoke City imemfuta kazi aliyekuwa kocha wake - Mark Hughes kutokana na mfululizo wa vipigo kwenye michezo mitano iliyopita.

Image may contain: 1 person, standing
Mark Hughes

Timu hiyo imeambulia vipigo vitano kwenye michezo saba ya ligi kuu ya England na kuifanya iteremke mpaka kwenye eneo la hatari la kushuka daraja na kumfanya kocha Hughes kuwa kwenye wakati mgumu kwenye kikosi hicho.