Matokeo ya Uchunguzi kuhusu Kakobe kutamka yeye ni Tajiri kuliko Serikali

Uchunguzi uliofanywa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kuhusu akaunti za benki zinazomilikiwa na Zachary Kakobe, Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel umeonyesha Askofu huyo hana akaunti binafsi kwenye taasisi yoyote ya fedha nchini. Kanisa lake tu ndio lina akaunti ambayo ina kiasi cha Shilingi Bilioni 8.
Serikali iliagiza uchunguzi baada ya Askofu kusema ana utajiri kuliko Serikali kauli ambayo aliifafanua baadae kupitia Biblia (Neno la Mungu).